Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anataka kununua mshambuliaji mpya kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu.
Huku mshambuliaji wao Olivier Giroud akiwa majeruhi, Arsenal walilazimishwa sare ya 1-1 na Leicester iliyopanda daraja, katika mchezo wa siku ya Jumapili, licha ya kupiga mikwaju 24 iliyolenga goli.
Baada ya mchezo huo, Wenger aliulizwa kuhusu safu yake ya ushambuliaji na alisema: "Tuko macho katika dirisha hili la usajili. Tunafanya kazi kwa nguvu kutafuta suluhu.
"Hakuna anayeweza kubashiri kitakachotokea katika saa 24 zijazo."
Giroud, ambaye alifunga mabao 16 ya Ligi Kuu msimu uliopita, amefunga magoli mawili msimu huu, na aliumia katika mchezo dhidi ya Everton wiki ikiyopita. Giroud hatocheza hadi mwishoni mwa Disemba, baada ya kufanyiwa upasuaji katika mguu alioumia.