come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MILOVAN CIRKOVIC KUMRITHI PHIRI SIMBA

Wakati siku za kocha mkuu wa Simba Mzambia Patrick Phiri zinahesabika, uvumi umeenea kuwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mserbia Milovan Cirkovic yuko mbioni kurejea Simba.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambacho kipo karibu na mabosi wa klabu hiyo kinasema kuwa Milovan ni chaguo la kwanza endapo ataondoka Phiri.

Milovan ni kocha mzuri aliyewahi kuibebesha ubingwa Simba mara kadhaa kilisema chanzo hicho. Aidha mabosi hao wamewaambia wanachama na mashabiki wa Simba wajiandae kupata furaha mara baada ya kuwasili kocha huyo.

Milovan atakumbukwa sana na mashabiki wa Simba hasa baada ya kuipa kipigo cha kihistoria Yanga cha mabao 5-0 ambacho hadi leo hakijasahaulika.


Phiri amekalia kuti kavu Simba hasa baada ya kuiongoza timu hiyo kucheza mechi 6 na zote ikitoka sare hivyo ikifikisha pointi 6.

Kocha huyo amebakiwa na kibarua kigumu kwani ameachiwa mechi moja tu dhidi ya Ruvu Shooting ambapo ametakiwa kushinda na endapo Simba itafungwa au kutoka sare atatimuliwa.