come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ACHENI KUJIFANYA WAJUAJI WA SOKA


Na Fikiri Salum



WASWAHILI wana msemo wao 'Mvumilivu hula mbivu' au ule mwingine 'Haraka haraka haina baraka', ni misemo tu ambayo inapaswa kutumiwa, hivyo ndivyo unavyoweza kusema hasa kuhusiana na sakata la usajili wa mabeki Joseph Zutta 'teteh' raia wa Ghana na mwenzake Vincent Bossou raia wa Togo ambao wananyooshewa vidole.

Zuttah yeye alitangazwa kuachwa na vyombo vya habari na nafasi yake kuchukuliwa na Vincent Bossou ambaye naye ameanza kuangaliwa kwa jicho la tatu na kuonekana hafai kuitumikia timu hiyo.

Hivi karibuni kumezuka tabia mbaya hasa kutoka kwa baadhi ya wanaojiita wachambuzi wa soka ambao hawana taaluma hiyo hata kidogo, na mashabiki pia wameingia kwenye mkumbo huo, ambapo wameanzisha kamtindo cha kumjaji mchezaji kwenye mechi moja, kwa mujibu na taratibu za mchezo wa soka. mchezaji hajadiliwi kwa mechi moja peke yake ili kupima uwezo wake.

Kuna madhara makubwa kumjadili mchezaji kwenye mechi moja, inawezekana ukajiridhisha kuwa umepata mchezaji bora na mahiri kwenye mechi moja hasa baada ya kumuona akifunga goli au kuwapiga wenzake chenga za maudhi, kanzu na tobo.

Ukaridhika naye na kuamjua kumpa mkataba, lakini mnaposhuka tena uwanjani kucheza mechi nyingine mchezaji huyo huyo anashindwa kuwaonyesha yale yale aliyoyafanya mwanzo, kumbe siku ile bahati nzuri ilikuwa kwake.

Na vile vile unaweza ukamleta mchezaji bora kabisa ambaye aling'ara kwenye michuano fulani, lakini mchezaji huyo ukampa mechi moja ya majaribio uwanja wa Taifa na akashindwa kuonyesha mambo yake yaliyomfanya atakiwe na klabu yenu.


Tayari maneno yameanza eti beki huyu raia wa Togo Vincent Bossou amekwisha

Baada ya mechi mnapitisha maamuzi kuwa hafai na mnamtimua, lakini mchezaji huyo huyo anang'ara kwenye timu nyingine itakayomchukua, ni vema tukaawachia wataalamu kwenye maamuzi ya wachezaji bora na si bora.

Makocha ndiyo wanaohusika na hilo na wao ndiyo wanaotambua uwezo wa mchezaji, lakini siku hizi tumekuwa tukiwasikia viongozi wakizungumzia utaalamu wa mchezaji, kiongozi haoni hasara akisema mchezaji fulani hafai na wanaamua kumkata ili mradi kuwafurahisha mashabiki wake.

Nimeangalia uwezo wa beki wa pembeni wa Yanga Joseph Zutta 'Teteh', nimegundua ni beki mzuri anayefaa kucheza nafasi hiyo na nyinginezo, siku zte mchezaji anahitaji kupewa muda ili aweze kuzoeana na wenzake.

Mchezaji anahitaji kuvumiliwa na kama hilo halitafanyika kwake mtamuona hafai hata Yaya Toure akija Yanga, Zuttah ni beki wa pembeni anayecheza namba mbili, ana uwezo mkubwa wa kupiga krosi zenye madhara na amefanya hivyo kwenye mechi mbalimbali alizocheza akiwa Yanga SC.

Ila baadhi ya wachambuzi kwa matakwa yao aidha kuingiza ushabiki wakaanza kumuandama Zuttah, na kumsema kwa mabaya, kilichotokea viongozi wa Yanga wakaanza kuingia hofu na kutaka kumrejesha kwao, Zuttah tayari alishasaini mkataba wa miaka miwili hivyo wangefanikiwa kuuvunja mkataba wake wangelazimika kumlipa na fidia.

Yanga walishapangiwa nafasi za kusajili na hao wachambuzi, waliambiwa wana pengo la beki wa kati na kiungo mkabaji, waliopo sasa yaani Kelvin Yondan na nahodha Nador Haroub 'Cannavaro' eti wamechoka kwa sababu wamecheza mechi nyingi sana ni huu ni wakati wao kupumzika, hilo si kweli ni unafiki tu wa watu.

Usajili wa Zuttah ulikuwa sahihi kwakuwa amekuja kusaidiana na Juma Abdul ambaye mara kwa mara amekuwa majeruhi, pia wakadai Yanga ina mapungufu sehemu ya kiungo mkabaji wakati si kweli, Yanga inao viungo Mbuyu Twite anayecheza namba sita na Haruna Niyonzima anayecheza namba nane, pia inao viungo wengine kama Salum Telela ambaye pia yupo timu ya taifa, Taifa Stars na Said Juma Makapu 'Kizota'.

Tukielezea kuhusu Yondan na Cannavaro eti kwamba wamechoka kwa kucheza muda mrefu hilo si kweli na ni propaganda za kuwamaliza, Yondan na Cannavaro hawana mechi nyingi kama ilivyo kwa mabeki wa ligi za Ulaya, ligi ya Tanzania mchezaji mmoja alikuwa anacheza mechi 26 ambazo ni ndogo mno.

Ligi ya Uingereza inashirikisha timu 20, mchezaji mmoja anacheza mechi 38, hapo bado kuna michuano ya FA na kombe la ligi ambayo kwa hapa kwetu haipo, TFF ikaamua kuongeza timu hadi 16 badala ya 14 ligi kuu bara lengo ni kuwaongezea ushindani wachezaji wetu.

Beki Nadir Haroub 'Cannavaro' bado yuko fiti, alkini wachambuzi wanasema amechoka

Cannavaro na Yondan wako katika viwango vya hali ya ju hivyo kuletewa beki mwingine mwenye uwezo kama wao kunapelekea kumuona hafai, lakini Vincent Bossou ni beki mzuri na ndio maana ameitwa kwenye timu ya taifa ya Togo kama ilivyo kwa Yondan na Cannavaro walioitwa Stars.

Usajili wa kiungo raia wa Zimbabwe Thabani Kamusoko ni chaguo la wachambuzi ambao walidai Yanga ina mapungufu kwenye idara hiyo, lakini ukiangalia kiundani Yanga haikuwa na mapungufu ya kiungo mkabaji kwani ilionao ni wengi na walitosha kwa kazi hiyo.

Uwezo wa Kamusoko ni mkubwa lakini hautofautiani na ule wa Mbuyu Twite, sasa unapohoji kiwango cha Kamusoko eti kwamba si lolote utakuwa umekosea, pia katika mchezo wa soka kuna faida moja ambayo ni kubwa, faida hiyo ni kuzoeana.

Ili uweze kugundua kipaji cha mchezaji lazima azoeane na wenzake na hapo ndio utaweza kujua uwezo wa mchezaji mpya, lakini kinachofanyika sasa katika usajili wa vilabu vetu vya Yanga na Simba ni machaguo ya watu wanaojiita wachambuzi ambao wanazitibulia klabu hizo katika kutafuta wachezaji wazuri na kudumu nao wachezaji wa zamani