come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SWANSEA YAIKATA MAINI MAN UNITED

Garry Monk 

Swansea City wameanza kuwa wababe Ligi ya Premia baada yao kuendeleza rekodi ya kutoshindwa tangu mwanzo wa msimu kwa kutoka nyuma na kulaza Manchester United 2-1, meneja wao Garry Monk amesema.

Ushindi wa Jumapili ulikuwa wa tatu mfululizo kwa Swansea dhidi ya United na uliendeleza mwanzo wao mwema wa msimu ulioanza kwa sare ugenini kwa mabingwa wa ligi Chelsea.

“Timu yetu ni nzuri sana,” Monk aliambia Sky Sports. "Tumeanza kuwika ligini na tunapokuwa sawa na kucheza vyema tunaweza kuwa wazuri ajabu.

“Tunapokuwa hatuchezi vyema zaidi tunaweza bado kucheza vyema na hilo ndile muhimu katika kuwa timu nzuri.”

Klabu hiyo ya Wales ilipandishwa daraja kujiunga na Ligi ya Premia 2011 na ilidhihirisha ubabe wake ligi kuu mwanzo chini ya Brendan Rodgers na baadaye Michael Laudrup.

Klabu hiyo ilishinda League Cup 2013, kombe lao la kwanza kubwa, lakini Laudrup alifutwa na nafasi yake ikachukuliwa na Monk aliyekuwa hana uzoefu mkubwa 2014 – kazi yake ya kwanza kama meneja.
Monk, hata hivyo, alishangaza kwa kuwaongoza kumaliza nambari nane msimu uliopita kwa kuzoa alama 56, ambayo ni rekodi kwao, na wameanza msimu huu kwa kishindo.

“Ni vile tu sisi hufanya kazi na mambo ambayo nimepanga na wachezaji uwanjani nan je ya uwanja. Huwa twafanyia kazi sana mtazamo wetu na jinsi tunaingia kwenye mechi,” alisema Monk, ambaye ameendeleza utamaduni wa klabu hiyo wa kudhibiti mpira sana, na kutoa pasi kwa ufasaha.


"Leo mliona sifa zetu na ufundi. Mmetazama katika mechi ambazo tayari tumecheza msimu huu tumecheza vyema sana na kwa njia tofauti na kuonyesha kila upande wa sifa zetu. Hilo ndilo klabu nzuri inafaa kuwa ikifanya.”

Muhimu zaidi kwa ushindi wa Jumapili ulikuwa uwezo wao wa kubadilika kuambatana na mechi.
Monk alianza mechi kwa mpangilio wa 4-2-3-1 bila mafanikio lakini akarejerea mpangilio wa almasi na kubadilisha mechi hiyo kwa mabao mawili ya haraka kutoka kwa Andre Ayew na Bafetimbi Gomis.
"Tulidhani walikuwa wakituzidia sana katikati kwa hivyo tukabadilisha na kuwa muundo wa almasi kwa dakika 10 kipindi hicho cha pili,” Monk aliongeza.

“Ninafikiri hilo lilitusaidia kupata mabao mawili ya haraka na mwishowe tulifanya tu mabadiliko kadha madogo na kumaliza mechi vyema.”

Mwenzake Monk upande ule mwingine Louis van Gaal alisema kushindwa kwa timu yake kubadilika kukabili mpangilio mpya wa Swansea kuliwagharimu mechi hiyo.
"Walianza na mpangilio wa 4-2-3-1 na baada ya mambo kuwa 1-0 walibadilisha umbo lao. Hatukuweza kukabili hilo na hilo si jambo njema.”