NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amempiku hasimu wake mkubwa, Cristiano Ronaldo na mchezaji mwenzake wa Baeca, Luis Suarez katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Ulaya msimu wa 2014-15.
Messi ameshinda tuzo hiyo mwa mara ya pili katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Monte Carlo mjini Monaco, Ufaransa jioni hii baada ya kupangwa kwa ratiba ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ujeruman,i Celia Sasic ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa Mwaka Ulaya akiwa tayari ametangaza atastaafu soka tangu mwezi uliopita.
Sasic amewapiku mchezaji mwenzake wa Ujerumani, Dzsenifer Marozsan na Amandine Henry wa Ufaransa alioingia nao fainali