Na Saleh Ally, Kartepe
Kikosi cha timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, sasa kitakuwa kikifanya
mazoezi mara moja tu kwa siku kuanzia juzi Jumamosi.
Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, amesema atafanya
hivyo ili kuepusha kuwachosha wachezaji.
“Hii ni kuepusha kuwachosha
wachezaji, maana tulifanya mazoezi kwa nguvu sana siku za mwanzo baada ya
kufika Uturuki,” alisema Mkwasa.
“Utaona hata mechi dhidi ya Libya pia ilikuwa nguvu na wachezaji
walipambana sana. Hivyo sasa tutachezea mpira na mambo ya kiufundi zaidi,”
aliongeza.