NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema anataka mshambuliaji wao mpya, Mzimbabwe Donald Ngoma aongeze mabao na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS-ONLINE jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Canavaro alisema hiyo ndiyo sababu alikataa kupiga penalti jana, Yanga SC ikishinda 3-0 dhidi ya Prisons Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakiwa wanaongoza 2-0, Yanga wakapata penalti dakika ya 60 na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm akamuita Cannavaro akapige, lakini beki huyo naye akaenda kumpa jukumu hilo Ngoma aliye katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe kutoka FC Platinum ya kwao.
Na Ngoma akaenda kufunga bao lake la sita tangu atue Jangwani katika mechi ya 11 na kuifanya Yanga SC ishinde mechi ya pili mfululizo naye akifunga mechi ya pili mfululizo, baada ya awali pia kufunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union Jumapili.
“Sijapingana na kocha, nilipenda Ngoma aipige ile penalti, ili aongeze mabao yake katika kuwania ufungaji bora. Na nilimuambia kocha akanikubalia,"amesema Cannavaro.
Mchezaji huyo kutoka visiwani Zanzibar alisema endapo Ngoma angekosa penati hiyo, basi angekubali kubeba lawama zote, kwani hakuchaguliwa na kocha Pluijm kufanya kazi hiyo.
Donald Ngoma (kushoto) alifunga kwa penalti jana Yanga SC ikishinda 3-0 dhidi ya Prisons Yanga SC inatarajiwa kushuka tena dimbani Jumamosi kumenyana na JKT Ruvu iliyofungwa mechi zote mbili za mwanzo Nyanda za Juu Kusini 1-0 na Majimaji na 3-0 na Mbeya City leo.
Baada ya hapo, wana Jangwani hao watakwenda kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC Septemba 26 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
Septemba 19, 2015
Stand United Vs African Sports
Mgambo Shooting Vs Majimaji FC
Prisons Vs Mbeya City
Yanga SC Vs JKT Ruvu
Septemba 20, 2015
Mwadui FC Vs Azam FC
Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
Simba SC Vs Kagera Sugar
Coastal Union Vs Toto Africans
Septemba 26, 2015
Simba SC Vs Yanga SC
Coastal Union Vs Mwadui FC
Prisons Vs Mgambo Shooting
JKT Ruvu Vs Stand United
Mtibwa Sugar Vs Majimaji FC
Kagera Sugar Vs Toto Africans
Septemba 27, 2015
African Sports Vs Ndanda FC
Azam FC Vs Mbeya City