Milipuko miwili imetokea kwenye mkutano wa hadhara kati kati mwa mji mkuu wa Uturuki , Ankara wakati watu walikuwa wamekusanyika kufanya maandamano ya amani.,
Vyombo vya habari vinasemna kuwa takriban watu 30 waliuawa.
Picha za televisheni zilionyesha watu waliokuw na hofu na wengine wakiwa wamelala chini wakiwa wamejawa damu.
Huku duru ya pili ya uchaguzi wa ubunge ikifanyika mwezi ujao , maandanmano hayo yalipangwa na vyama vya wafanyikazi wakitaka kumalizika kwa mashambulii yanayoendeshwa na serikali dhidi ya wanamgambo wa kurdi.