come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

FIFA YAKUBALI OKWI KUKIPIGA YANGA.

MUDA wowote kuanzia sasa shirikisho la kandanda duniani linatarajia kutoa maamuzi mazito kwa klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia ambayo imeshindwa hadi sasa kuilipaklabu ya Simba fedha zake za mauzo ya mchezaji Emmanuel Anord Okwi jumla ya shilingi milioni 480 ambazo ni sawa na dola 300,000 za kimarekani.

Tayari CAF imemruhusu Okwi kuichezxea Yanga katika michuano ya kimataifa ambapo sasa FIFA nayo inatarajia kumruhusu straika huyo ghali kabisa katika ukanda huu wa Afrika mashariki, FIFA itafungua milango kwa Okwi kuitumikia klabu yake mpya ya Yanga kuichezea kwa ajili ya ligi kuu kufuatia klabu yake ya zamani ya Etoile Du Sahel ya Tunisia kuvunja mkataba kisheria.

Kwa mujibu wa vifungu vya sheria vya FIFA na CAF, Mchezaji asipolipwa mshahara wake miezi mitatu ni sawa na kuvunjwa kwa mkataba wake, Okwi hajalipwa mshahara wake wa miezi mitatu na kuamua kurejea kwao Uganda ambapo klabu ya SC Villa iliamua kumuomba kwa kupewa kibali maalum na FIFA kitakachomfanya acheze kwa miezi sita na ikimalizika atakuwa huru kwenda kokote anapooataka.


Kwa namna hiyo Okwi yuko huru kuichezea Yanga kulingana na sheria za kimataifa za FIFA, pia klabu ya Etoile Du Sahel inatakiwa kuilipa Simba fedha inazodai huku adhabu kali dhidi yake ikitolewa ikiwemo ile ya kutofanya usajili wowote kwa sasa.