come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Neymar anyimwa ushindi mechi ya kwanza Barca

Neymar

Mchezaji mpya wa Barcelona Neymar alikosa ushindi mechi yake ya kwanza alipoingia kutoka benchi kipindi cha pili cha mechi ya kirafiki dhidi ya Lechia Gdansk ya Poland iliyoisha sare ya 2-2 mnamo Jumanne.

Fowadi huyo kutoka Brazil aliyeng’aa sana wakati wa ushindi wa taifa lake Kombe la Confederations mwezi uliopita, alijiunga na wachezaji wenzake mnamo Jumatatu na akasafiri hadi Poland kuchezea Barca kwa mara ya kwanza tangu ajiunge nao kutoka Santos.
Aliingia uwanjani kuchukua pahala pa fowadi kutoka Chile Alexis Sanchez dakika ya 78, muda mfupi tu baada ya Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani Lionel Messi kuondolewa pia uwanjani, na alikaribishwa kwa changamoto kali kutoka kwa wachezaji wenyeji.
Kocha mpya Gerardo Martino hakusafiri na timu hiyo Poland na atajiunga na benchi Barca itakapokuwa mwenyeji wa klabu ya zamani ya Neymar kwa mechi ya kirafiki uwanjani Nou Camp mnamo Ijumaa.
Kulikuwa na dakika moja ya kimya kabla ya mechi hiyo mjini Gdansk baada ya Barca kutangaza awali Jumanne kwamba golikipa wao wa zamani Antoni Ramallets alikuwa amefariki akiwa na umri wa miaka 89.
Ramallets alichezea klabu hiyo ya Catalona mara 473 kati ya 1946 na 1961 na akashinda mataji sita ya La Liga na matano ya Kombe la Uhispania.
Alitunukiwa tuzo ya Zamora ya golikipa bora zaidi wa La Liga mara tano na alikuwa kwenye kikosi cha Uhispania kilichomaliza nambari nne Kombe la Dunia la 1950 nchini Brazil.