Timu ya Newcastle inatafuta kwa udi na uvumba kuapata siani ya mshambuliaji wa Wigan Arouna Kone.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29
alishinda magoli 11 katika ligi kuu ya England na kushinda kombe la FA
lakini anataka kuihama timu hiyo baada ya kushushwa daraja.NewCastle ina upinzani wa Evarton ambayo nayo imekuwa ikitaka kumsajiri.Lakini Meneja wa Wigan Owen Coyle amesema mshambuliaji huyo kutoka IvoryCoast , yeye anagependelea kuhamia Everton.
"Ninaamini kupitia mwakilishi wake kuwa Everton ndiko anakotaka kuhamia"alisema Coyle.
Arouna Kone alisaini mkataba wa miaka mitatu alipojiunga na Wigan kutoka Levante ya Uhispania msimu uliopita na alikuwa kwenye kikosi kilichonyakua ushindi mkubwa wa kwanza kwa timu hiyo,waliposhinda Manchester City goli 1-0 katika fainali ya kombe la FA mwezi Mei mwaka huu.