come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

CHELSEA YAMNYATIA LAVEZZI

KLABU ya Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji wa Paris St Germain, Ezequiel Lavezzi.

Klabu hiyo ya Ufaransa imemsajili David Luiz na inawataka pia Eden Hazard, Oscar na Petr Cech, wachezaji wengine wa Chelsea pia.

Tayari katika majadiliajo yao inafahamika Chelsea imeuliza bei ya kuuzwa kwa Muargentina Lavezzi ambaye ana nia ya kucheza michuano ya ushindani zaidi.

Chelsea inasaka mshambuliaji kama Samuel Eto'o kuingizwa katika orodha ya wachezaji wa kutemwa, na inafikiriwa wameelekeza nguvu zao kwa Lavezzi pamoja na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa.


Jose Mourinho pia anamtaka mchezaji ambaye Manchester City pia wanamtaka, kiungo wa ulinzi Eliaquim Mangala wa Porto baada ya kugionga mamba kwa Raphael Varane wa Real Madrid.