come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

CHUJI, LUHENDE HAWAJAACHWA YANGA

Na Regina Mkonde

UONGOZI wa mabingwa wa Ngao ya Hisani Yanga umesema nyota wake Athuman Idd 'Chuji' na David Luhende hawajatemwa na kikosi hicho mpaka pale watakapopitia mapendekezo ya kocha wao aliyeondoka Mholanzi Hans Van Der Pluijm.

Tayari baadhi ya vyombo vya habari vimeanza kuvumisha kuwa Yanga imewatema nyota wake hao ambao wanatangazwa kujiunga na Simba, kiongozi mmoja wa Yanga ambaye ndiye chanzo chetu cha habari amesema jana kuwa Yanga haijatangaza wachezaji inaowatema.

'Chuji na Luhende bado ni mali ya Yanga licha ya mikataba yao kuelekea ukingoni, tutatoa tamko maalum kama tumewaacha au tunaendelea nao kwakuwa ripoti ya kocha inaendelewa kufanyiwa kazi, mpaka sasa Yanga imeongeza mkataba wa mchezaji mmoja tu ambaye ni Mbuyu Twite.


Huku nyota wengine saba wakiwa hawajui hatma yao kama wataendelea kuitumikia klabu hiyo msimu ujao unaotarajia kuanza Agosti 24, Wachezaji Ally Mustapha 'Barthez', Athuman Idd 'Chuji', David Luhende, Said Bahanuzi, Deogratus Munishi 'Dida', Hussein Javu na Juma Abdul hawajui hatma yao ingawa taarifa za ndani zinasema Abdul na Dida wataongezewa mikataba mapema iwezekanavyo.

Wakati Chuji, Luhende na Barthez wanadaiwa kujiunga na Simba huku tetezi nyingine kuwa mlinda mlango mashuhuri nchini Juma Kaseja naye anadaiwa kurejea timu yake ya zamani ya Simba kufuatia Yanga kutokuwa na imani naye