![]() |
|
|
|
Straika mkuu wa Uruguay, Luis Suarez, atafanyiwa
upasuaji gotini lake Alhamisi katika harakati za kumwezesha kushiriki
Dimba la Dunia ambalo limesalia majuma matatu pekee.
Taifa lake lilipigwa na kiwewe baada ya mshabuliaji huyo aliyeshamiri pakubwa musimu huu na klabu cha Uingereza, Liverpool, kuumiza goti lake kwenye kambi ya mazoezi kulingana na duru za wanahabari.
Suarez, aliyeoongoza Uruguay kufuzu semifainali ya Dimba lililotangulia Afrika Kusini alitarajiwa kuwa nyota wa timu kwenye kinyang’anyiro kinacho anza Juni 12 hadi Julai 13 Brazil.
Kulingana na kituo cha runinga, Tenfield, mshabuliaji huyo, 27, alipigwa picha ya MRI Jumatano iliyoonesha jeraha la goti ambalo daktari wa timu hiyo aliamua mara moja kuwa upasuaji unahitajika.
Jeraha kama lake linachukua siku 15 hadi 20 kupona kulingana na taarifa hiyo kumaanisha Suarez hatakuwa na muda wa kutosha kunoa makali kabla ya Uruguay kujitosa uwanjani katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Costa Rica, jijini Fortaleza mnamo Juni 14.
Unigereza na Italia wanakamilisha Kundi D linalokisiwa kula la ‘kifo’.