come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MR IBU ATOA NENO...........

Na Regina Mkonde aliyekuwa Nigeria

Msanii maarufu wa tasnia ya filam kutoka Nigeria John Okafor maarufu kama Mr Ibu hivi karibuni alifunguka na kuwaasa wasanii hususani wa kike kuto toa miili yao kwa ajili ya kupata umaarufu bali wajitahidi kufanya kazi kwa bidii.

Ingawa kuna baadhi ya watu walitoa hoja na kudai kuwa si jambo la ajabu kwa producer kutembea na msanii kauli hii iliongelewa na msanii maarufu wa Nollywood anayefahamika kwa jina la Aniedi Noba na kusema kuwa ikiwa producer na msanii wa kike wote ni watu wazima na wana hisia si ajabu kwa wao kuwa wapenzi.

Mr Ibu ambaye alianza shughuli za uigizaji mnamo mwaka 1978 na kupata mafanikio makubwa katika sanaa ambaye alishawahi kuchukua tuzo nyingi nje na ndani ya Nigeria John Okafor alikuwa msanii wa kwanza wa kinigeria kutwaa tuzo ya mchekeshaji bora wa filamu za kiingereza za kiafrika .zilizotolewa jijini London Uingereza mwaka 2002/2003

.
Pia Mr Ibu alipata tuzo miaka miwili mfululizo mwaka 2005 na 2006 katika tuzo za za mchekeshaji bora wa filam za kiingera Afrika(Best Comedy Actor in English film in Africa) licha ya tuzo hizo mara kibao alizoa tuzo nyingi za msanii bora wa vichekesho nchini Nigeria.

Hivi sasa gwiji huyo wa Filam za vichekesho anatarajia kutoa filam mpya ambayo hakuitaja jina rasmi na kudai kuwa kisa cha kutotaja jina la filam hiyo kwa sasa ni kutokana na uharamia uliokithiri kwenye soko la filam la Nollywood.

Mr Ibu ambaye alitamba na filam inayoitwa Mr Ibu ambayo aliigiza na msanii maarufu Osita Iheme(Moo/Paw paw) aliigiza kama baba wa Moo filam hii ilizidi kumpa jina msanii huyu na kufahamika nje ya Afrika kwa ujumla.

Licha ya hivyo Mr Ibu alieleza jinsi sanaa ya Nigeria ilivyokuwa na kutanua wigo wake alisema kwamba hapo awali kulikuwa na vifaa duni vya kutendea kazi na havina ubora.Hapo awali   tulikuwa tunatumia kamera moja wakati wa kurekodi kazi ila hivi sasa tunatumia zaidi ya kamera moja kwenye shooting.

‘Ingawa hatujafikia kiwango cha wenzetu wan je ila kidogo tumeendelea wenzetu hutumia kamera 20 wakati wa kufanya shooting  ya filam moja.’Aliongea Mr Ibu.Kitu ambacho kinamkwaza msanii huyo kwenye tasnia ya filam nchini Nigeria ni tatizo la usambazaji wa kazi za filam ambapo kuna maduka matatu tu ambayo yanasambaza kazi za wasanii changamoto hii hupelekea kazi zao kutofika sehemu nyingi.

‘Kitu ambacho kama nitapata uwezo nitahakikisha naboresha usambazaji na kufungua kampuni ambayo itashughulika na mambo ya kusambaza kazi za wasanii.

Mr Ibu alidai kuwa yeye bado atabaki kuwa mchekeshaji bora Afrika nzima na atazidi kuachia filam kali na hatowaangusha wadau wa kazi zake.

Pia aliwashauri wasanii ambao wanaingia kwenye sanaa kwa ajili ya maslahi ya pesa badala ya kazi sababu chanzo kinachopelekea kwa wasanii wa kike kuuza utu wao ni kutaka umaarufu wa haraka na kutajirika badala yake wazidi kumuomba Mungu ili awape mafanikio yaliyo yaharari.

‘Usitoe mwili wako sababu ya kuwa maarufu wala usitoe pesa sababu unataka umaarufu hali hii ndiyo inyaofanya soko la sanaa lishindwe kuendelea Nigeria’Mr Ibu alisema.Mr Ibu hivi sasa ni baba wa watoto watano ambapo mtoto wake mdogo ana umri wa mwaka mmoja licha ya hivyo Mr Ibu anasikitika kwa kmpoteza mtoto wake mmoja ambaye alitekwa na watu wasiojulikana.