03/05/2013
Na Majuto Mbiligenda
KIUNGO machachari wa mabingwa wa zamani wa bara Simba SC, Mrisho Khalfan Ngassa hatimaye sasa ameonekana kuigeuka klabu yake hiyo baada ya kukubali kutua Yanga.
Ngassa (Pichani juu na chini) amekubali kujiunga na mabingwa wapya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga msimu ujao ambapo sasa takabidhiwa jezi yake upya.
Taharifa za kukubali rasmi na kujiunga na Yanga zimepatikana mapema leo ambapo duru za klabu ya Yanga kuendelea kufanya naye mazungumzo kutokana na mkataba wake na Simba kumalizika mwezi huu.
Ngassa ameonyeshwa kufurahishwa na vibopa wa klabu ya Yanga kumuongezea dau jipya tofauti na lile walilokubaliana hapo awali.
Dau hilo (Halijatajwa) inaonekana ni kubwa pamoja na mshahara mnono ambao utavunja rekodi ya wachezaji wote hapa nchini na kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi nchini.
Hivyo amewataka mashabiki wa Yanga kutokuwa na wasiwasi na tayari yuko mbioni kurejea katika klabu yake ya zamani ya Yanga.
Ingawa anarejea tena Yanga, Ngassa anasema kuwa nafurahia sana kurudi Yanga kutokana na matatizo makubwa aliyokuwa akiyapata Simba wakati ikifanya vibaya katika mechi zake za ligi kuu na michuano ya kimataifa ambapo lawama zote alikuwa akibebeshwa yeye