LICHA ya kuwa kinara wa kuvaa uhusika wa ukahaba na tabia zisizokubalika katika jamii bila kujali yanayosemwa na watu, safari hii mambo yamekuwa ni tofauti kwa mwigizaji, Tonto Dike.
Ameamua kuweka bayana sababu ya kukubali
kuigiza filamu ya ‘Dirty Secret’ ambayo Tonto anaigiza kama msichana
aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba yake licha ya kuwa na mpenzi
mwingine.
Nafasi ya baba katika filamu hiyo
inaigizwa na Jibola Dabo aliyecheza kama baba mwenye mahusiano ya
kimapenzi na binti yake. Nafasi ya mpenzi wa binti yake ikichezwa na
Muna Obikwe.
Katika filamu hiyo mastaa hao watatu, kila
mmoja alifanikiwa kucheza vizuri katika nafasi yake jambo lililochangia
ujumbe kufika kwa usahihi.
Pamoja na ukweli huo, jamii ya Wanigeria
ilikuwa na maswali mengi juu ya kwanini hasa mastaa hao waliamua kuigiza
filamu hiyo wakidai haina uhusiano na utamaduni wa Wanigeria.
Katika mahojiano yake aliyoyafanya hivi
karibuni, Tonto ameweka bayana sababu ya yeye kuigiza filamu hiyo akidai
ni simulizi yenye maudhui ya kweli.
“Dirty Secret ni simulizi ya kweli kwani
hata msichana aliyetokewa na mkasa huo nilikutana naye na ndio maana
nikaguswa na kuicheza nafasi hiyo," alisema Tonto.