BAYERN Munich (Pichani) imetwaa Super Cup ya Ulaya
 baada ya kuifuna Chelsea kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 na Jose 
Mourinho ameshindwa kutwaa taji la kwanza baada ya kurejea darajani 
mbele ya Pep Guardiola.
Katika mchezo huo, ambao Chelsea ilimaliza pungufu baada ya Ramires kutolewa nje kwa nyekundu dakika ya 84, mabao ya The Blues yalifungwa na Torres dakika ya nane na Hazard dakika ya 93, wakati ya Bayern yalifungwa na Ribery dakika ya 47 na Javi Martinez dakika ya 120.
Katika mikwaju ya penalti, Ashley Cole alifunga Cech akaokoa penalti Xherdan Shaqiri. 
Penalti nyingine zilizofungwa na David
 Luiz, Oscar na Frank Lampard kwa upande wa  Chelsea, wakati za Bayern 
zilifungwa na Jerome Boateng, Toni Kroos, Philipp Lahm na Franck Ribery 
hivyo kuteneneza ushindi wa 5-4. 
Kikosi cha Bayern Munich 
kilikuwa: Neuer, Rafinha/Javi Martinez dk56, Dante, Boateng, Alaba, 
Muller/Gotze dk70, Lahm, Kroos, Ribery, Mandzukic na Robben/Shaqiri 
dk95.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Ramires, Lampard, Hazard, Oscar, Schurrle, Torres/Lukaku dk97
