Baadhi ya viongozi wa Coastal Union ya Tanga wameonyessha masikitiko yao kupinga maamuzi mabaya yaliyotolewa dhidi ya pambano lao la ligi kuu kati yao na Yanga uliochezwa siku ya jumatano iliyopita ambapo timu hizo ziligawana pointi moja moja baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Akizungumza katiika kipindi cha michezo cha redio One Stereo, Msemaji wa Coastal Union ya Tanga Edo Kumwembe alidai kitendo cha mwamuzi wa mchezo huo Martin Saanya kuwapa penalti kiliwashangaza hata wao kwani licha ya kutafuta goli la kusawazisha lakini ile haikuwa penalti ya halali.
Kumwembe alisisitiza kuwa hata Yanga wameduwazwa kufungwa dakika ya mwisho wa mchezo yaani tisini, 'Ile haikuwa penalti hata sisi tulishangaa lakini ndio maamuzi', alisema Kumwembe, Pia alilalamikia kadi nyekundu aliyopewaOdullo badala ya Banda.
Kumwembe amewataka waamuzi kuchezesha kwa weledi na kuacha kutumia sheria mkononi, Yanga wamepeleka malalamiko yao TFF kupinga maamuzi mabovu yaliyotolewa na Saanya