Wapiganaji wa M23
Waasi wa M23 Mashariki mwa
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema kuwa watasitisha mapigano,
kufuatia makabiliano makali na wanajeshi wa serikali wanaoungwa mkono na
wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.
Afisa mmoja wa Kundi hilo la M23 Museveni Sendugo, ameiambia BBC kuwa wanajeshi wake tayari wamerudi nyuma umbali wa kilomita tano kutoka eneo la mapigano.
Kiongozi wa kundi hilo Bertrand Bisima amesema uamuzi huo utaruhusu wachunguzi huru kupeleleza jinsi makombora yalivyorushwa nchini Rwanda siku ya Alhamisi.
Serikali ya Rwanda imesema jeshi la Congo lilirusha makombora hayo, madai ambayo yamekanusha na serikali ya Congo.
Wengi wa wapiganaji wa M23 ni wanajeshi walioasi jeshi la serikali, wengi wao wakiwa wa kibila la Kitutsi sawa na uongozi wa Rwanda.
Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa zimeishutumu serikali ya Rwanda kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa kundi hilo la M23, tuhuma ambazo zimekanushwa na utawala wa Kigali.za amani nchini DRC, Monusco, kiliimarishwa zaidi pale wanajeshi elfu tatu zaidi walipotumwa nchini humo kupambana na waasi hao.
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo, amesema mabomu na makombora kumi na tatu yalirushwa katika ardhi yake siku ya Jumatano na mengine kumi siku ya Alhamisi.