KLABU ya Arsenal inatumai kumaliza miaka tisa ya kusubiri saini ya Gonzalo Higuain wiki hii kwa kuweka rekodi ya dau lake la usajili, Pauni Milioni 22 ofa waliyotoa kumnasa mshambuliaji huyo.
Muargentina huyo amekubali kuhamia Emirates majira haya ya joto na The Gunners - ambao pia wanaamini watambakiza beki Bacary Sagna na Laurent Koscielny kuelekea msimu ujao - wiki hii itafanya mipango rasmi ya kumsaini nyota huyo wa Real Madrid, ambaye ameambiwa yuko huru kuondoka Bernebeu.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger yuko tayari kumwaga fedha kusajili
Mazungumzo baina ya viongozi wa Arsenal
na wawakilishi wa Higuain yanaendelea vizuri na inasemekana kilichobaki
ni klabu hizo mbili kukubaliana.
Kwa sasa dau kubwa la usajili walilowahi
kutoa ni Pauni Milioni 15 kwa Zenit St Petersburg kumsajili Andrey
Arshavin, Arsenal iko tayari kumpa mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki
Higuain.
The Gunners imekuwa ikimmezea mate
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 tangu akiwa River Plate, timu yake
ya kwanza mwaka 2004.
Amechuja: Andrey Arshavin amechemsha Arsenal licha ya kushikilia rekodi ya kusajiliwa bei mbaya
Arsenal ilijaribu uwezekano wa kumsajili Muargentina huyo mzaliwa wa Ufaransa mwaka 2006, lakini wakazidiwa kete na Real Madrid.
Lakini Wenger anatarajiwa kukata kiu yake ya muda mrefu kwa mshambuliaji huyo, Higuain hivi karibuni.
Arsenal imeendelea na nia yake thabiti
ya kutaka kuwasajili Wayne Rooney na Stevan Jovetic, lakini dili la
Higuain ndilo la ukweli zaidi.
Mtutu mdogo? Arsenal pia inataka kumsajili mchezaji wa U21 ya Hispania, Asier Illarramendi (katikati)
Wakati huo huo, The Gunners wanaongoza
mbio ya kuwania saini ya nyota wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri
wa miaka 21 ya Hispania, Asier Illarramendi.
Kiungo huyo wa ulinzi wa Real Sociedad
mwenye thamani ya Pauni Milioni 10 anang'ara kwa sasa na anaitoa udenda
na Real Madrid pia.
Arsenal pia inamfuatilia Gilbert Imbula - lakini Illaramendi akuwa sahihi zaidi akicheza na Mikel Arteta.