Mabingwa hao wa Ufaransa walitaka Mreno
huyo arithi mikoba ya Carlo Ancelotti, anayeelekea Real Madrid, lakini
sasa wamehamishia mawindo yao kwa Fabio Capello.
Inafahamika Villas-Boas alipewa ofa ya
Mkataba wa miaka mitatu na mabilionea wa Qatari wanaoimiliki PSG baada
ya majadiliano na wakala wake, Carlos Goncalves, lakini mwalimu huyo
kijana wa miaka 35 anataka kufanya mambo adimu Spurs waliomchukua msimu
uliopita baada ya kutupiwa virago Chelsea.
Anabakit: Villas-Boas ameripotiwa kubaki White Hart Lane
Kazi ya kufanya: Villas-Boas anataka kuipaisha matawi ya juu zaidi Spurs kutoka nafasi ya tano aliyowapa msimu uliopita
Tottenham wanatarajiwa kubomoa benki
kumpa fedha za kutosha Villas-Boas, aliyebakiza miaka miwili katika
Mkataba wake White Hart Lane, ili kujenga kikosi cha nguvu cha kukata
tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
Miongoni mwa wachezaji anaowataka ni
kiungo wa Corinthians, Paulinho, wakati Spurs pia ni klabu pekee
iliyoomba kumsajili kiungo wa Atletico Mineiro, Bernard. Wakala wake
amesema: "Dortmund hawajawasilisha mapendekezo na Tottenham ni
washindani pekee,".
Villas-Boas pia inaelezwa anavutiwa na
ushindani wa kupambana na bosi wake wa zamani, Mreno mwenzake Jose
Mourinho katika Ligi Kuu England msimu ujao.
Taarifa za jana usiku nchini Ufaransa
zinasema kocha wa zamani wa England, Capello atakuwa mwalimu mpya wa PSG
kwa Mkataba wa mwaka mmoja.
Kocha wa zamani wa England, Capello anatazamiwa kuwa mpango B wa PSG, licha ya kwamba bado ana Mkataba wa mwaka mmoja Urusi.
Urusi ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu
kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil,na kuna
uwezekano Capello akarejea katika timu hiyo ya taifa baada ya msimu
mmoja na PSG kukamilisha majukumu yake katika Kombe la Dunia.
Carlo Ancelotti anatarajia kuhamia Real Madrid
Msimu mzuri: PSG walikuwa mabingwa Ufaransa na wanataka kujiimarisha zaidi