KOCHA
Andre Villas-Boas atataka uhakika juu ya Tottenham kumbakiza Gareth
Bale na kupewa fungu la kusajili wachezaji anaowataka kabla ya kujifunga
katika klabu hiyo.
Mreno huyo anatakiwa na
Paris Saint-Germain akachukue nafasi ya mwalimu anayehamia Real Madrid,
Carlo Ancelotti.
Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy anataka kumbakiza kocha wake huyo wa thamani ya juu White Hart Lane msimu ujao.
Lakini
Spurs wanafahamu Villas-Boas akienda PSG lazima kocha huyo wa zamani wa
Chelsea agharimiwe Pauni Milioni 10 za kuvunja Mkataba.
Wakuu wa Tottenham wanaamini mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 35 anataka kubaki na kukamilisha kazi yake aliyoianza Spurs.
Lakini
inafahamika AVB yuko katika nafasi ya kutumia kuhitajiwa kwake na PSG
kuushinikiza uongozi utimize matakwa yake majira haya ya joto.
Kuhakikishiwa
kubaki kwa Bale, anayetakiwa na PSG na Real Madrid, ndio kipaumbele cha
Villas-Boas kipindi hiki, lakini pia anataka kuboresha safu yake ya
ushambuliaji.
Hatari: Aidha nyota Gareth Bale abaki ili Villas-Boas abaki, au waondoke wote.
David Villa na Roberto Soldado wote wanahitajiwa, wakati Spurs inammezea mate kwa muda mrefu Leandro Damiao.
And
Villas-Boas anataka kuhakikishiwa Levy anafanya jitihada za kuhakikisha
anakamilisha mapendekezo yake kabla hajaamua mustakabali wake.