KLABU ya Tottenham inataka kukata Pauni Milioni 15 kwa ajili ya kiungo Mbrazil, Paulinho kupambana na Roma na Inter Milan ili kuinasa saini yake.
Mpango huo unakuja baada ya Fenerbahce kufufua nia ya kumnunua mshambuliaji Emmanuel Adebayor ambaye atawasaidia kupata fedha.
Paulinho,
mwenye umri wa miaka 24, ambaye jina lake kamili ni Jose Paulo Bezerra
Maciel Junior, alitarajiwa kusaini kwa moja ya timu za Italia wiki hii
baada ya kufikia makubaliano ya awali.
Pamoja na hayo, nyota huyo wa Corinthians inaelezwa anapenda kuhamia Ligi Kuu ya England.
Tottenham
inaweza kutakiwa kupanda dau kidogo hadi Pauni milioni 18 pamoja na
kwamba wanahamasika na kujua mchezaji huyo anapenda kuhamia London.
Akizungumza
nchini Brazil, Naibu Mkurugenzi wa Corinthians, Duilio Monteiro Alves,
alisema: "(Tottenham) ni klabu ambayo tunafahamu ina nia, lakini bado
hakuna kitu rasmi kilichofanyika. Dhahiri itakuja. Tunatarajia siku
zijazo.
"Lengo letu ni kumzuia, lakini acha tusubiri na tuone; ikiwa ni nzuri kwake, nzuri kwa Corinthians, tutafanya uamuzi,".
Anatakiwa muda mrefu: Leandro Damiao amekuwa akitakiwa kwa muda mrefu Tottenham
Kiungo
wa Atletico, Mineiro Bernard, mwenye umri wa miaka 20, pia anatakiwa na
mshambuliaji wa Internacional, Leandro Damiao anabaki kuwa suluhisho
wakati Mbrazil mwingine, beki kinda wa miaka 18 wa Botafogo, Doria,
amekuwa akijadiliwa.
Paulinho amezivutia Roma, Inter na Tottenham, lakini amesema hatatoa uamuzi hadi baada ya Kombe la Mabara.
Kuwasili
kwake White Hart Lane kutafungua milango ya watu kuondoka Spurs, kama
inavyofahamika Fulham inamtaka Tom Huddlestone na mkongwe mwenye umri wa
miaka 32, Scott Parker, ambaye anatakiwa Sunderland.
Wanaondoka? Tom Huddlestone na Scott Parker wanaweza kuondoka Tottenham
Anaondoka? Emmanuel Adebayor anaweza kuuzwa Spurs
Adebayor
ni kati ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi katika klabu hiyo na
kuondoka kwake kutasaidia kufanikisha kwa dili nyingine.
Fenerbahce
ilijaribu kumsaini mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 29 kabla
wakati akiwa bado Manchester City na inatarajia kufanikisha mpango wake
safari hii.