MSHAMBULIAJI Mario Balotelli atakutana ana kwa ana na wachezaji wa timu yake ya zamani baada ya AC Milan kupangwa na Manchester City katika Nusu Fainali za Kombe la Audi mjini Munich.
Mshambuliaji huyo mtata wa Italia
alirejea San Siro Januari mwaka huu kwa dau la Pauni Milioni 19, baada
ya miaka mitatu ya kuitumikia Manchester City.
Sasa anatarajiwa kuivaa klabu yake ya
zamani kwa mara ya kwanza Julai 31 katika mashindano ya kujiandaa na
msimu mpya Uwanja wa Allianz Arena.
Uhamisho mkubwa: Balotelli alitua AC Milan akitokea Manchester City kwa ada ya Pauni milioni 20
Wenyeji na mabingwa wa U;aya, Bayern
Munich watacheza na Sao Paulo ya Brazil katika mchezo wao mwingine wa
Nusu Fainali jioni hiyo hiyo.
Balotelli amekuwa katika kiwango kizuri
tangu arejee Italia akifunga mabao 12 katika mechi 13 za Serie A ikiwa
ni zaidi ya mchezo mmoja kutoka mechi 14 alizocheza mzunguko wa kwanza
England.
Balotelli akiwapigia makofi mashabiki