KOCHA wa Simba, Abdalah Kibadeni ameshikwa na
kigugumizi kutangaza kikosi kipya cha timu hiyo atakachokitumia msimu
ujao na sasa atafanya hivyo baada ya kurejea kwa baadhi ya wachezaji
wake walioko kikosi cha taifa, Taifa Stars.
Katikati ya wiki hii, kocha huyo alisema ataweka
hadharani majina ya wachezaji atakaowahitaji na wale atakaoachana nao
kwa ajili ya msimu ujao.
Akizungumza na mtandao huu jana, Kibadeni alitaja
sababu ya kushindwa kufanya hivyo kuwa bado anahitaji muda zaidi wa
kuwapima wachezaji hao kutokana na wengi wao kuwa wapya.
“Ni ngumu kwa sasa kujua mchezaji yupi ni bora kwa
kufanya mazoezi tu.,” alisema Kibadeni na kuongeza: “Mchezaji lazima
acheze mechi kadhaa za majaribio ndipo unaweza kupana nafasi nzuri ya
kujua kiwango chake.”
“Ni vigumu katika muda mfupi kuweza kugundua kiwango cha mchezaji kwa sababu, kuna mambo mengi yanapaswa kuangalia kwa muda mrefu.”
“Ni vigumu katika muda mfupi kuweza kugundua kiwango cha mchezaji kwa sababu, kuna mambo mengi yanapaswa kuangalia kwa muda mrefu.”
Tunahitaji mechi zaidi za kujipima nguvu na kuwa karibu na wachezaji kwa muda,” alisema Kibadeni.
Kibadeni amesema anasubiri maombi kwa uongozi wa klabu hiyo kupata mechi za kirafiki ili aweze kujua viwango vya wachezaji wake.