KIUNGO aliyeleta mageuzi makubwa katika klabu ya Simba ambaye hivi karibuni alitajwa kusaini Yanga kabla hawajafanya tahimini vizuri na kumsainisha mkataba wa miaka miwili jana Amri Kiemba hatimaye amepata dili nyingine ya kutakiwa kucheza soka la kulipwa Morocco.
Kwa mujibu wa taharifa zilizotolewa jana na viongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa mwenyekiti wake Ismail Aden Rage, Zinasema kuwa Kiemba anahitajika nchini Morocco na klabu ya Raja Casablanca iko tayari kumchukua mchezaji huyo ambaye alikuwa gumzo katika mchezo kati ya timu ya taifa, Taifa Stars ilipocheza naMorocco jumamosi iliyopita.
Rage amesema kuwa timu ya Raja Casablanca imevutiwa na kiwango cha Kiemba na iko tayari kuilipa Simba ili kumchukua nyota huyo, Kiemba ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars na yuko kambini kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Ivory Coast utakaochezwa jumapili ijayo.
Endapo mchezaji huyo atasajiliwa na Raja ataweka pengo kubwa katika klabu yake ya Simba kwani tayari imeshaondokewa na wachezaji wake nyota Emmanuel Okwi, Kelvin Yondani na Haruna Moshi 'Boban' aliyejiunga na Coastal Union ya Tanga.
Mwanzoni mwa wiki hii, Kiemba alizua gumzo kubwa kufuatia habari zilizoenea kuwa amejiunga na Yanga na amesaini kwa mkataba wa miaka miwili jambo ambalo Yanga ilikanusha vikali, Simba jana imekamilisha kuingia naye mkataba wa miaka mwili baada ya kuafikiana naye