Manchester City wamepatwa na msiba mzito, baada ya Paka wao anayejulikana kama 'Wimblydon' kufariki dunia kutokana na uzee.
Huyu
paka ana sifa za kipekee, aliwahi kumletea Kevin Keegan panya aliyekufa
ofisini kwake, na inaaminika ndiye kiumbe hai wa kwanza kumpokea Mario
Balotelli alipojiunga na timu hiyo akitokea Inter Milan.
Mario Balotelli na Paka Wimblydon |
Paka huyo 'alijiunga' na staff ya Citizen mwaka 1999, na inasemekana ameshakula panya zaidi ya 200 pamoja na lita 100 za maziwa.
Wimblydon, Manchester City Cat, 1999 (est) – June 11, 2013