Leiwing ambaye aliajiriwa na Simba baada ya Simba kumtimua aliyekuwa kocha wa timu Mserbia Milovan Cirkovic mara baada ya kuisha kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita na kumuajiri Mfaransa Leiwing kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu. Leiwing aliiongoza Simba katika mzunguko wote wa pili na kuiwezesha Simba kushika nafasi ya 3 nyuma ya mabingwa Yanga na washindi wa pili Azam FC. Lakini mara baada tu ya ligi kuisha kocha huyo akaondoka kwenda kwao kwa mapumziko lakini akiwa huko uongozi wa Simba ulitangaza kumtema na kumuajiri aliyekuwa kocha wa Kagera Sugar Abdallah King Kibaden.
Kwa taarifa zilizothibitishwa na gazeti la Mwananchi ni kwamba Leiwing ametua nchini leo na kusisitiza kwamba hatambui suala la kuachishwa kazi na Simba.
Kwa taarifa zaidi kuhusu ujio wa kocha huyu endelea kutembelea mtandao huu utapata mengi zaidi