Mkuu wa Kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni ya Rockstar 4000 Bi. Christine Mosha “Seven” akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo |
Nexus Consulting Agency imenunua haki zote za usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi la hilo la Komedi ambalo kwa miaka kadhaa sasa limekuwa namba moja katika sanaa ya uchekeshaji. Mkataba huu utakuwa kwa ajili ya kusimamia kipindi cha Orijino Komedi kuweza kuendelea kuwa namba 1 Tanzania na pia kupanua utazamwaji wake nje ya mipaka ya Tanzania.
Mkataba wa Orijino Komedi na Nexus umetajwa kuwa ni wa kuanzia miaka miwili mpaka mitano.
"Kushirikiana na Orijino Komedi ni kitu muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao kutokana na vipaji vyao vya hali ya juu wanavyovionyesha kundi hilo,' alisema mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bobby Bharwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Nexus Consulting Agency Bw. Bobby Bharwani (kushoto) |