come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NELSON MANDELA ALINUSA KIFO, MADAKTARI WASEMA


Ni siku nne zimepita imetokea hali ya sintofahamu baada ya mpiganiaji Uhuru wa Afrika Kusini mzee Nelson Mandela kukimbizwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya na kuwekwa kwenye chumba cha watu mahututi.


Ripoti kutoka kwenye hospitali aliyolazwa Rais huyo wa zamani wa Taifa hilo inasema usiku wa kuamkia leo siku ya Alhamisi majira ya saa 8 usiku hali ya Mandela ilibadilika tena.

Ndipo Timu ya madaktari ilikusanyika na yalionekana Mapigo ya Moyo kuacha kufanya kazi kwa muda na Figo kushindwa kufanya kazi kwa dakika zisizopungua 10.

Baada ya kupigania uhai wake hali ilirudi kuwa ya kawaida na kuendelea
kupata matibabu chini ya madaktari bingwa.

Pia Rais wa sasa wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameongea na kusema 'ninaamini timu ya madaktari inayomuangalia mzee wetu na nina imani mungu atamuepusha na mabaya yote na kurudi kwenye hali yake kama kawaida, Nampenda mzee Mandela', Alisema na kuongeza.

Wanachi wa Afrika Kusini Wote tunampenda Mandela na dunia nzima inampenda kwahiyo kwa pamoja tuungane kumuombea', alimaliza Zuma ambaye ni rais wa tatu mzalendo wa nchi hiyo iliyotoka kwenye utawala wa makaburu ambapo mzee Mandela alilikomboa taifa hilo baadaya kutumikia kifungo cha miaka 25 jela