KLABU ya Marseille imethibitisha nia yake ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast anayechezea Arsenal, Gervinho ambaye ametua jana Dar es Salaam na timu yake ya taifa kwa ajili ya mechi na Tanzania Jumapili.
Rasta
huyo mwenye umri wa miaka 26, aliigharimu Arsenal Pauni Milioni 11
aliposajiliwa kutoka Lille na amekutana na wakati mgumu katika Ligi Kuu
ya England.
Kocha
Msaidizi wa Marseille, Franck Passi amesema: "Huu ni wasifu ambao
unatuvutia, ndiyo. Tunataka wachezaji wa pembeni, wenye uwezo wa
kuchezea mpira, kutoa pasi na kufunga na Gervinho ana wasifu huu,".
Tangu
asaini Arsenal mwaka 2011, Gervinho ameifungia mabao 11 klabu hiyo ya
Kaskazini mwa London, machache mno ukilinganisha na winga mwenzake, Theo
Walcott aliyefunga mabao 32 katika muda huo.
Na
Arsene Wenger akiwa tayari kutumia kiasi cha Pauni Milioni 70 katika
pazia la usajili, Gervinho pengo lake linaweza kuzibwa na mchezaji wa
bei kubwa, kama nyota wa Fiorentina, Steven Jovetic au Gonzalo Higuain
wa Real Madird.
Gervinho
anaweza kuporomoka zaidi msimu ujao kutokana na Alex Oxlade-Chamberlain
kutarajiwa kupewa nafasi zaidi katika kikosi cha kwanza.
Barafu iliyoyeyuka: Wenger amempasha Gervinho wazi kwa kiwango cha chini kilichomkatisha tamaa