MSHAMBULIAJI mpya wa Barcelona,Neymar jana aling'ara katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mabara, akifunga bao la mapema dakika ya tatu wakati Brazil inailaza 3-0 Japan.
Mshambuliaj
huyo nyota wa Brazil, alifunga kwa shuti la nje ya eneo la hatari,
akiunganisha pasi ya Fred ambaye naye alipokea krosi ya Marcelo kwa
kifua kwanza.
Paulinho alifunga la pili dakika ya 48 kwa pasi ya Dani Alves na Jo akafunga la tatu dakika ya 90.
Ushindi
huo unaiweka Brazil kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake tatu. Italia
na Mexico watamenyana leo katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Kikosi cha Brazil jana kilikuwa; Julio
Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Oscar, Gustavo,
Paulinho, Fred/Jo dk81, Neymar/Lucas Moura dk74 na Hulk/Hernanes dk75.
Japan: Kawashima,
Konno, Nagatomo, Uchida, Yoshida, Endo/Hosogai dk77, Honda/Inui dk88,
Kiyotake/Maeda dk51,Kagawa, Hasebe na Okazaki.
Chukua hiyo: Neymar aling'ara jana
Nyota wa Chelsea, David Luiz akishangilia na wenzake