BAADA ya kukamilisha uhamisho wake kutua
Barcelona, Neymar ambaye anaungana na Lionel Messi kuunda safu mpya
kali ya ushambuliaji, ameweka wazi malengo yake.
Mbrazil huyo alisafiri moja kwa moja
kwenda Hispania baada ya Brazil kutoa sare ya 2-2 nyumbani na England
mjini Rio de Janeiro Jumapili, na katika mahojiano aliyofanyiwa kwenye
Uwanja wa Nou Camp alisema: "Nipo tayari kumsaidia Messi kuendelea
kuwa mchezaji bora duniani,".
Neymar alipokewa kifalme katika Uwanja
wa Ndege wa Barcelona - kabla ya kupelekwa kwenye ofisi za klabu hiyo
kwa ajili ya kupigwa picha akiwa na jezi ya Blaugrana kisha kwenda
kufanyiwa vipimo vya afya.
Neymar alitambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Barcelona Nou Camp jana
Mbrazil huyo amesaini Mkataba wa miaka mitano Catalan.
Neymar anaungana na 'mchawi' huyu Lionel Messi kuunda safu kali ya ushambuliaji Barcelona