Amedai kuwa yeye tayari amesaini kuichezea Yanga na akili zake zote amezielekeza Jangawani, Amewataka mshabiki wa Yanga kokote walipo kuachana na uzushi huo ambao umeenezwa na watu wachache wenye lengo la kutaka kumvuruga yeye pamoja na Yanga.
Ngassa amesisitiza kuwa yeye ni mchezaji halali wa Yanga na suala la kurejea Simba kwa sasa halipo, TFF kwa kutambua mkataba wake na Yanga haiwezi kuidhinisha aichezeee Simba wakati hana mkataba na timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi.
Ngassa alimaliza mkataba wake wa kuichezea Simba kwa mkopo mwezi Mei mwaka huu na alisajiliwa rasmi na mabingwa wa Tanzania bara Yanga kwa ajili ya kuitumikia katika msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom pamoja na michuano ya kimataifa mwakani