come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Rihanna kimenuka

 
BABA mzazi wa mwanamuziki, Chris Brown aitwaye, Clinton Brown, amesema habariki uhusiano wa mwanaye na mwanamuziki mwenzake, Rihanna kwa kuwa binti huyo anaonekana hajatulia.
Brown alisema uhusiano wa Chris na Rihanna hauwezi kudumu kwa kuwa ni wa mafahari wawili, lakini alimsifia ‘mkewe’ huyo kuwa ni mrembo na mwenye mafanikio.
Anasema mwanamke anayemfaa Chris Brown ni mpenzi wake wa zamani, Karrueche Tran kwa kuwa binti huyo alikuwa mtulivu na mnyenyekevu tofauti na Rihanna.
Aliongeza kuwa kama Chris anapenda kuwa na mwanamke, ambaye ni mwanamuziki kama yeye, basi Jordin Spark angemfaa kwa kuwa ni mrembo, ana kipaji na mtulivu pia.