come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Serikali yakosa mwendeshaji Uwanja wa Taifa

Leonard Thadeo
Serikali bado haijapata kampuni inayokidhi vigezo ili kuingia nayo ubia wa kuendesha Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam, imeelezwa.

Akizungumza kwenye ofisi za makao makuu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo alisema kuwa bado wanaendelea kusaka kampuni ya kuendesha uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watu 57,558.

"Bado tunaendelea na mchakato wa kutafuta mtu au kampuni yenye uwezo wa kuendesha uwanja wetu, tukishakamilisha tutawajulisha," alisema Thadeo bila kutaja kampuni ambazo tayari zimeshajitokeza kuomba zabuni hiyo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo, Juliana Yassoda naye hakutaka kuweka wazi kampuni zilizochangamkia zabuni hiyo huku akisema kuwa kuna kampuni nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza lakini hawajaipata yenye sifa wanazozihitaji.

"Wengi wamejitokeza tangu tulipotangaza tenda hiyo lakini bado hatujapata kampuni sahihi ya kuuendesha. Wengine wanakuja, tunaongea nao lakini wanaenda na hawarudi tena kuendelea na mazungumzo," alisema Yassoda.

Serikali kupitia wizara yenye dhamana ya michezo nchini imekuwa ikitoa matangazo ya kusaka kampuni kwa ajili ya kuuendesha uwanja huo pindi tu kampuni ya Beijing Construction ya China itakapoukabidhi kwa serikali
ilianza kujenga Uwanja wa Taifa mwaka 2005 lakini hadi sasa bado haijaukabidhi rasmi kwa serikali.

Februari 15, 2009 Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, Hu Jintao, aliyekuwa amefuatana na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete, aliuzindua rasmi uwanja huo.

Kila mechi ya klabu na timu za taifa inayochezwa katika uwanja huo, serikali hupata asilimia 15 ya mapato baada ya makato ya kodi, mbali na ingizo jingine kupitia makato mbalimbali yakiwamo ya Kodi la Ongezeko la Thamani  (VAT).