Warembo 18 kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mwanza wamejitokeza kushiriki shindano hilo.
Warembo wote wanatarajiwa kuanza kambi rasmi kesho Jumanne katika moja ya hoteli maarufu jijini humo.
Katika kumbukumbu la shindano la Miss Tanzania
Mkoa wa Mwanza una historia za kutoa washindi akiwamo mrembo wa
Tanzania, ambaye ni Nasreem Karim 2009 na Miriam Gerald 2010.
Pamoja na mchakato wa shindano la urembo kuendelea
hivi sasa nchini, macho na masikio yapo mkoani Mwanza ambako kumekua
kukileta changamoto na upinzani mkali kwa warembo kila mwaka.
Sugu atasindikizwa na mwanamuziki mwingine nguli
kutoka katika Kundi la TMK ‘Wanaume Family,’ Juma Said maarufu kama
Chege Chigunda.