Akizungumza na Mwananchi Nyamwela anayeshambulia
jukwaa kupitia Bendi ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo, alisema hivi
sasa amekamilisha wimbo mpya Dullee Duvellee ambao ameuimba kwa staili
ya Bongo Pop.
“Hii ni staili mpya kabisa ya muziki hapa nchini,
wimbo huu nimerekodi katika studio za C91 Records, zilizopo Kinondoni,
nimemshirikisha msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mukky kutoka katika
Kundi la Makomandoo lililo chini ya uangalizi wa Tanzania House of
Talent THT,” alisema Nyamwela.
Pia lisema baada ya kukamilisha wimbo huo mpya yupo katika mipango ya kuzindua staili yake mpya ya Bongo Pop.
‘’Staili mpya ya Bongo Pop, inakwenda na ‘Swaga za
Duvellee Duvellee’ ambayo kwa Kiswahili cha mtaani ni Shwari Shwari, na
tayari wimbo huu nimeusambaza katika vituo mbalimbali vya redio nchini
na baadhi vimeanza kuutendea haki kwa kuupiga na kuwapa raha
wasikilizaji,’’ alisema Nyamwela.
Pia Nyamwela amesema yupo katika maandalizi ya kurekodi video ya wimbo huo