Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara
Hadi sasa, tayari wanamichezo kutoka katika kanda 11 za Tanzania
Bara na moja kutoka Zanzibar wameshawasili mjini hapa kushiriki
mashindano hayo.
Afisa Michezo na Utamaduni Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Mohamed
Kiganja, alisema kuwa ufunguzi rasmi utaanza saa 7:00 mchana kwenye
viwanja vya Shule ya Sekondari Kibaha, ukitanguliwa na gwaride la
wanamichezo wote watakaoshiriki mashindano hayo.
"Michezo ya netiboli itahusisha timu za wasichana pekee na mchezo
wa bao utahusisha timu za wavulana tu... michezo mingine yote iliyobaki
itawashirikisha wavulana na wasichana," alisema Kiganja, huku akiitaja
baadhi ya michezo mingine kuwa ni kikapu, riadha, wavu, mpira wa mikono
na soka," alisema Kiganja.