Uongozi wa bendi ya Twanga Pepeta (Pichani) umebuni mbinu kali
ya kupeleleza kambi za wapinzani wao kwa kutumia baadhi ya wanamuziki
wake waaminifu kwa nia ya kukomesha vitendo vya kuwachukulia nyota wao
bila kufuata taratibu halali.
Mkurugenzi wa kampuni ya Aset inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, ndiye aliyeanika 'janja' hiyo hivi karibuni, akidai kuwa baadhi ya wanamuziki wake ni kama virusi ambao wamekuwa wakijipenyeza kwenye bendi nyingine kwa nia kuchukua siri za huko.
Bosi huyo wa Twanga alikaririwa akisema hayo wakati akijibu shutuma dhidi yake kutoka kwa mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo kuwa anaifuatilia sana bendi hiyo.
"Wapo wasanii wamelelewa vizuri, wamefanyiwa mengi na Twanga, wanaelewa utu. Akiwafuata atapoteza pesa zake bure... wanatuletea taarifa za kila mtu anayetaka kuwaachukua," alisema Asha ambaye amekuwa katika mgogoro mkubwa na Choki wa Extra Bongo kuhusiana na madai ya kuchukuliana wanamuziki.
Uhasama huo ulikolezwa hivi karibuni baada ya mpiga gita mmoja wa Twanga kudaiwa kusaini mkataba wa kuitumikia Extra Bongo na kupewa Sh. milioni 5, lakini mwishowe akaingia mitini na kubaki Twanga.