MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Lukas Podolski
ataukosa mchezo wa Jumapili wa wapinzani wa London Kaskazini, dhidi ya
Tottenham baada ya kuumia nyama katika mchezo wa Ligi ya Mabinwa jana
dhidi ya Fenerbahce.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerymani
anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia katika
dakika za mwanzoni za kipindi cha pili kwenye ushindi wa 2-0 katika
mchezo huo wa marudiani, hivyo timu yake kusonga mbele hatua ya makundi
kwa ushindi wa jumla wa 5-0 dhidi ya Waturuki.
Kocha Arsene Wenger amesema: "Tmetugharimu mno kwa majeruhi hayo, kwa sababu tunampoteza Podolski.
"Podolski atakuwa nje kwa wastani wa siku 21,"alisema.
Aaron Ramsey alifunga mabao yote katika
usiku huo Arsenal ikijikatia tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi
ya Mabingwa kwa mara ya 16 mfululizo.
Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa
Wales naye pia alikuwa miongoni mwa wachezaji walioumia, akitoka nje
kabla ya mwisho wa mchezo na kuiacha Gunners ikimalizia mechi na
wachezaji 10.
Kiungo Jack Wilshere pia naye alipatwa na misukosuko, alipokabiliana na Raul Mereiles na Bruno Alves, na kumuachia maumivu.
Majanga juu ya majanga: Jack Wilshere aliumia kifundo cha mguu, lakini akaendelea na mechi Arsenal ikiifunga Fenerbahce
Wenger alisema: "Sifahamu kiasi gani
Ramsey ameumia. Sifahamu Wilshere anaendeleaje. Tutaangalia hiyo kesho
(leo) asubuhi. Makwanja mawili kwa Wilshere yalisikitisha, lakini anaonekana yuko sawa.
"Jack atakuwa sawa Jumapili. Natumai hivyo kwa Aaron pia. Nilimuona akitoka nje zikiwa zimesalia dakika tatu au nne mechi kumalizika, lakini sijui anajisikia vibaya kiasi gani. Alitaka kubaki uwanjani,".
Wenger alitaka kumtoa nje Wilshere,
kutokana na historia ya matatizo ya maumivu ya kifundo cha mguu kwa
mchezaji huyo, lakini mchezaji huyo akaamua kuendelea kucheza.
"Nilitaka kumtoa nje, ndiyo," Wenger alisema.
Shujaa wa mabao: Aaron Ramsey aliondoka uwanjani kabla ya mwisho wa mechi kutokana na maumivu ya nyonga
"Ilibidi tucheze na wachezaji 10.
Tulikuwa mbele kwa mabao 2-0, walitakiwa kufunga mabao matano ndani ya
dakika 10. Hata tulipobaki na wachezaji 10 tungeweza kuepuka hilo,".
Huku tayari wachezaji wake wengine,
Mikel Arteta na Alex Oxlade-Chamberlain wakiwa majeruhi, huu ni mtihani
mwingine kwa Wenger katika siku za mwishoni za pazia la usajili.
Kuna taarifa Juan Mata mkubwa, baba na wakala wa kiungo wa Chelsea, alikuwa Uwanja wa Emirates jana kuangalia mechi hiyo.
Anatakiwa: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa na nia ya kumsajili nyota wa Chelsea, Juan Mata
Kufuatia kiungo huyo wa Hispania
kupoteza namba katika kikosi cha kwanza Chelsea katika mechi dhidi ya
Manchester United usiku wa Jumatatu, tetesi zinasema anaweza kuuzwa.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amekanusha taarifa hizo na Wenger anaamini itakuwa shughuli pevu.
"Nampenda yeye,"alisema Wenger, ambaye
alizidiwa kete katika kuwania saini ya mchezaji huyo wa zamani wa
Valencia na Chelsea miaka miwili iliyopita.
"Niliangalia mechi hiyo jana (juzi) na
nimesikia, kama wewe, Juan Mata anaweza kutiwa sokoni,"alisema Wenger
ambaye hata hivyo anaamini klabu zinazoshindania ubingwa ni vigumu
kuuziana wachezaji zenyewe kwa zenyewe.