come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

CANNAVARO AICHIMBA MKWARA COASTAL UNION

Nahodha wa mabingwa wa soka nchini Yanga Nadir Haroub Ally 'Cannvaro' (Pichani) ameichimba mkwara mzito timu ya Coastal Union ambao jioni ya leo wanakutana kwenye uwanja wa Taifa katika raundi ya pili ya ligi kuu bara.


Cannavaro ametamba kuwa ni lazima Yanga iibuke na ushindi katika mchezo wa leo na amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi, Aidha beki huyo aliyesimama imara katika nafasi yake karibu misimu saba sasa amedai Yanga ni timu bora kuliko zote 13 zinazoshiriki ligi hiyo.

Hivyo ametambia ubora wa kikosi chake na kuahidi ushindi, 'Tunajua Coastal ni timu nzuri na tunaiheshimu lakini Yanga tuna kila sababu ya kuibuka washindi', alisema Cannavaro ambaye pia ni beki wa timu ya taifa, Taifa Stars.

Yanga ilianza kwa kishindo ligi kuu ya bara baada ya kuilaza Ashanti United mabao 5-1 wakati Coastal ikipata ushindi mdogo dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha