come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

AZAM MEDIA KUIJAZA MAMILIONI YANGA, ITAONGOZA KWA MKATABA MNONO

HUENDA kampuni mpya ya Azam Media ikafanikiwa kuijaza klabu ya Yanga (Pichani) mamilioni ya fedha baada ya kupatikana kwa suluhu dhidi yao hivi karibuni imebainika, kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kinasema kuwa Yanga inaweza kuwa klabu ya kwanza hapa nchini kupata udhamini mnono kutoka kwa kampuni hiyo.


Hivi karibuni serikali kupitia wizara yake ya habari na michezo illiitaka kamati ya ligi pamoja na wadhamini wapya wa kuonyesha mechi za ligi kuu msimu huu Azam Media kukaa meza moja na Yanga ambayo ilikataa kuikubali kampuni hiyo.

Kamati ya ligi na Azam Media zilikubali agizo la serikali na kukaa meza na Yanga ambapo waliweza kuelewana na kufikia sehemu muafaka, kwa sasa Yanga inaweza kuigia mkataba mnono na kampuni hiyo na inaweza kuizidi klabu ya Simba ambayo ilianza kuingia mkataba na Azam Media.

Hata hivyo Yanga mbali ya kusaini mkataba huo mnono itakubaliana na matakwa ya Azam Media kurusha mechi zake huku ikikubali kuchukua mgao wa milioni 100