come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

WAKANUSHA KUONDOKA KIIZA JANGWANI

UONGOZI wa mabingwa wa soka nchini Yanga jana umekanusha vikali habari zilizoenea kuwa mshambuliaji wake raia wa Uganda Hamis Kiiza (Pichani) anatarajia kuondoka nchini siku ya jumamosi mara baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam na kuelekea Lebanon ambapo amepata timu ya kuichezea.


Kwa mujibu wa msemaji wa timu hiyo Baraka Kizuguto, amesema kuwa Yanga haina taarifa hizo na inashangaa habari hizo kuenezwa kwa kasi mno, 'Hatujawa tayari kulizungumzia hilo kwa sasa lakini ikifikia tutasema' , alisema Kizuguto maarufu kama Kizu.

Hata hivyo Kizuguto alikuwa akiweka mkazo mechi yao dhidi ya Azam ambayo itachezwa siku ya Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Taifa kuwania Ngao ya Jamii, taarifa zilizosambazwa jana kupitia mitandao ya kijamii zinasema kwamba Kiiza anakwenda kucheza soka la kulipwa nchini Lebanon na kuwashangaza mashabiki wa Yanga ambao wamefurahishwa na ujio wake Yanga.

Kiiza aliongeza mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga hivyo taarifa za kuondoka kwake zimewachanganya sana Wanayanga, Mshambuliaji huyo alikuwa tegemeo katika kikosi hicho ambapo katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya bara msimu uliopita alifanikiwa kuifungia Yanga bao la pili la ushindi dhidi ya mtani wake wa jadi Simba.