Awali mechi hizo zlilipaswa kuanza kuonyeshwa leo wakati ligi ikianza, lakini kutokana na
kutosainiwa kwa mkataba rasmi, sasa zoezi hilo
limesimamishwa mpaka katika mzunguko wa nne kupisha umaliziaji wa
mazungumzo baina ya TFF na uongozi wa Azam.
Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana
kuwa nakubaliano kati ya pande hizo mbili yalifikiwana na ukasainiwa
mkataba wa awali ambao si rasmi (MoU) na kutakiwa
kusainiwa mwingine ambao utaruhusu urushwaji wa mechi ‘live’.
Katika hatua nyingine Wambura alisema tayari benki ya CRDB ambayo ndiyo ilishinda tenda
ya tiketi imeshakamilisha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya matumizi ya tiketi za kielektroniki hizo katika viwanja vyote.
“Hivi sasa Serikali ambayo ndiyo inamiliki Uwanja wa Taifa, TFF pamoja na CRDB
zinashughulikia mfumo wa tiketi hizo kwenye uwanja
huo ambao ndiyo ulikuwa haujakamilika kwa matumizi katika upande huo,”
alisema Wambura.