|
|
Baada ya miaka mitatu iliyofafanuliwa na Jose Mourinho
akibeza yeyote katika utawala wake Real Madrid, hali ya utulivu imetanda
katika klabu hicho miezi michache iliyopita kutokana na kuteuliwa kwake
Carlo Ancelotti kama meneja.
Raia huyo wa Italia amepokelewa kwa furaha na waandishi wa habari na kikosi chake kilichojaa nyota.
Wakati uwezekano wa Rais wa klabu, Florentino Perez, akiwaza ikiwa atavunja rekodi ya dunia ya kusajili mchezaji Gareth Bale, Madrid wameendelea na shughuli zao uwanjani kwa njia ipasayo.
Wameshinda mechi sita kati ya saba za kirafiki na sare moja huku kutwanga kwao Chelsea wanaotawaliwa na Mourinho, Paris Saint- Germain na Inter Milan ukivutia.
Lakini uhusiano uliozorota katika siku za mwisho za Mourinho na hatua za Perez katika soko zinamwacha Ancelotti na wakati mgumu kufanya maamuzi huku msimu wa Madrid ukingoa nanga wiki chache zijazo.
Huku Perez akionyesha umaahiri wa kusajili nyota wa siku za usoni, Isco na Asier Illarramendi kutoka kikosi cha chini ya miaka 21 cha Uhispania, viungo hao wapya hawatarajiwi kuanza mechi mara kwa mara.
Real walimimina kitita cha Euro milioni 69 kwa wawili hao lakini watapata ushindani kumiliki nafasi za kuanza kutoka wakongwe kama Mesut Ozil na Xabi Alonso.
Fauka ya hayo, ijapokuwa Perez ameonyesha dhahiri ya kusajili Bale, kuuza Gonzalo Higuain Napoli kumewacha mabingwa hao mara tisa wa kombe la klabu bingwa bara Uropa bila washambuliaji huku Karim Benzema na Alvaro Morata aliye na miaka 20 wakibakia kuongoza kitengo hicho.
Kufuatia tetesi zinazohusu Bale anayecheza katika muundo kamili wa nyota wa Madrid, Cristiano Ronaldo, kumemfanya Ancelotti amchezeshe staa huyo kama mshambuliaji wa kati katika mechi za kirafiki.
Hapo awali, Ronaldo ameelezea kutorithishwa kwake na kucheza katika nafasi hiyo, san asana na kikosi chake cha kitaifa Ureno lakini ikizingatiwa Madrid wanamshawishi nyota huyo kusaini mkataba mpya, haionekani kwamba kutakuwa na shinikizo lolote kwake kubadilisha kitengo.
Katika lango, Ancelotti ana kibarua cha kuamua nani kati ya nahodha Iker Casillas na Diego Lopez aliyepata Baraka za Mourinho msimu jana atapata nafasi ya kipa wa kwanza wa Madrid.
Licha ya malalamiko kutoka umma kufuatia masaibu ya Casillas, hakuna anayeweza kupinga kuwa Lopez hakustahili nafasi baada ya maonesho ya kusisimua kuelekea mwisho wa msimu.
Katika safu ya walinda ngome, Pepe ambaye alitiwa jokufu baada ya kulalamikia shida zilizomkumba Casillas hadharani alidaiwa na Mourinho kugadhabika kutokana na kupoteza nafasi yake kwa Raphael Varane mwenye unri wa miaka 20.
Pepe anakusudiwa kuanza kwa wiki chache zijazo huku Varane akiuguza jeraha lakini utulivu wa staa huyo wa umri wa miaka 30 unaweza kukatizwa iwapo atachaguliwa nyuma ya Mfaransa huyo na raia wa Uhispania, Sergio Ramos, kati ya ngome.
Dani Carvajal ametishia kumgatua Alvaro Arbeloa, mmoja wa wakereketo waliomuunga mikono Mourinho, katika nafasi ya beki wa kulia baada ya Real kuchukua fursa ya kumsajili tena kutoka Bayer Leverkusen wa Ujerumani.
Kufikia sasa, Ancelotti amejipata katika ziwa la utulivu lakini mambo yanaweza chacha pindi msimu utakapoanza dhidi ya Betis Jumapili.