come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

GOR MAHIA WAPIGWA STOP UWANJA WA MOI KASARANI



Mibambe wa Ligi Kuu Kenya, Gor Mahia, kwa mara ingine tena wamepigwa marufuku kuchezea mechi zao katika uwanja wa kimataifa wa Moi, Kasarani na ule wa Nyayo jijini Nairobi kwa muda usiobainika.
Hatua hii inajili baada ya visa vya machafuko vilivyo sambaratisha mwisho wa mechi yao dhidi ya Nairobi City Stars ugani Kasarani Agosti 4 iliyotamatika kwa sare tasa.
Gabriel Komora, ambaye ni Afisa Mkuu Mtendaji wa muda wa usimamizi wa viwanja vya michezo hapa nchini, alituma taarifa kwa wanahabari akielezea marufuku hiyo.
Fauka na hayo, aliwasilishia Gor gharama ya uharibifu ya kitita cha shilingi milioni 2.8 kufidia hasara iliyosababishwa katika vurumai hizo.
Taarifa hiyo inasoma, “Bodi ya usimamizi wa viwanja vya michezo imepiga marufuku klabu cha Gor Mahia kutumia viwanja vya Nyayo na ule wa kimataifa wa Moi, Kasarani.
“Uamuzi huu unajili kutokana na machafuko yaliotokea katika mechi yao na Nairobi City Stars Agosti 4 ambapo mashabiki wa Gor walizua rapsha na kuharibu mali nyingi ikiwemo viti, ua la uwanja na lango.”
“Bodi inaamuru Gor Mahia wawasilishe mpango kabambe wa vile wanavyokusudia kukabiliana na mashafuko kati ya mashabiki wao. Mpango huo ni lazima pia uoneshe wazi kwamba klabu hicho kiko tayari kutwaa jukumu la mashabiki wao kila wanavyohusika na visa kama hivyo,” taarifa hiyo iliongeza.
Kufuatia hatua hiyo, hatima ya kivumbi kikuu kinachotarajiwa kati ya Gor na maasimu wao wa jadi, AFC Leopards ambacho kilikuwa kimepangiwa uga wa Kasarani kimekumbwa na utata mkuu.