Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu amesema kuwa Niyonzima mara kwa mara amekuwa akiwasiliana na familia yake inayoishi huko Rwanda huku akiwa na wasiwasi juu ya kutokea kwa machafuko, Rais Poul Kagame wa Rwanda amekuwa na malumbano ya muda mrefu na rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kiasi kwamba kupelekea kutokuelewana kati ya nchi hizo mbili zilizokuwa na uhusiano mkubwa.
Kutokana na hofu hiyo kunaweza kukamweka shakani mchezaji huyo ambaye amekuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha timu ya Yanga, Huenda nyota huyo akatoweka nchini na kutafuta timu katika nchi nyingine ili kuhofia usalama wake ambao tayari ameuweka shakani.
Rafiki huyo wa karibu wa mchezaji huyo ambaye amektaa kutaja jina lake amedai kuwa msimamo wa Niyonzima kwa sasa ni kuona anaondoka nchini na kuelekea ughaibuni ili kutuliza akili yake kwani ana kumbukumbu na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyotokea Rwanda miaka kadhaa iliyopita