KUNGO wa kutumainiwa wa mabingwa wa zamani wa bara Simba SC Mwinyi Kazimoto (Pichani), ameivuruga klabu yake ya Simba baada ya kutoroka na kufanikiwa klupata timu nchini Qatar.
Kazimoto ambaye alitoroka kwenye kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda katika michuano ya kufuzu fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.
Mchezaji huyo alitoroka nchini na kutimkia Qatar ambapo inasemekana alikwenda kwa lengo la kufanya majaribio katika klabu moja inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
Kazimoto alifuzu majaribio hayo ambapo klabu yake aliyojiunga nayo imetuma ofa ya kutaka kumnunua, Taarifa za chiini chini zinasema kuwa uongozi wa Simba umeipuuza ofa hiyo kwa madai ni ndogo mno.
Simba ilitangaza kumpiga bei Kazimoto kwa kiasi cha shilingi milioni 160, Lakini klabu hiyo ya huko Qatar imetangaza dau dogo ambalo hata hivyo halikuwekwa wazi